MAMA DIAMOND AMFUMUA MOBETTO, ADAI ATAENDELEA KUMCHAPA

amshukia Mobetto, adai ataendelea kumchapa

Bingwa - - MBELE -

SANURA Kassimu maarufu kama Bi Sandra ambaye ni mama mzazi wa Diamond Platnumz, amedai mwanamitindo, Hamisa Mobetto, ameingia katika familia yake kwa lengo la kuvuruga kwa kuleta unafiki.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya tetesi kusambaa mtandaoni kuhusu Hamisa Mobetto kushushiwa kichapo na mama Diamond, baada ya kukutwa na Diamond nyumbani kwake Madale, Dar es Salaam.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Bi Sandra ambaye amekuwa akiupinga uhusiano wa kimapenzi wa Diamond na Hamisa Mobetto kuwa atahakikisha mwanawe hamuoi mwanamitindo huyo, kwani hana hadhi ya kuolewa na mwanawe licha ya kuwa wana mtoto mmoja, Daylan.

“Nitampiga kila atakapokuja Madale, kwani ni nyumbani kwangu na ninachagua watu wa kuja si kila uchafu uje tu na kuingia, hapa si hadhi yake, sikatai Naseeb kuoa ila si kwa Hamisa, akiendelea kujipendekeza kwenye familia yangu sitamuacha, nataka apaone Madale kama kituo cha polisi,” alisema mama Diamond.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.