Jamii Academy yasaka vipaji vya kikapu

Bingwa - - HABARI - NA GLORY MLAY

KLABU ya mpira wa kikapu ya Jamii Academy ya mkoani Dodoma, inaendelea kusaka vipaji vya wachezaji chipukizi wenye umri wa kuanzia miaka minne hadi minane ambao watashiriki michuano ya kitaifa na kimataifa kwa baadaye.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha wa klabu hiyo, Benson George, alisema wanasaka vipaji hivyo baada ya agizo lililotolewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa.

Rais huyo aliitaka mikoa kuandaa timu nyingi za vijana zitakazoshiriki mashindano mbalimbali.

“Bado tunapokea wachezaji wenye umri wa kuanzia miaka minne hadi minane, tunawaomba wazazi wawape watoto nafasi ya kuja kujifunza katika klabu yetu.

“Pia tunataka kuhakikisha Mkoa wa Dodoma unakuwa na timu nyingi za vijana kama sehemu ya kukuza mchezo wa kikapu,” alisema.

Aidha, aliongeza kuwa anaamini wachezaji chipukizi wenye vipaji waliokosa nafasi ya kuonekana, watapata fursa kupitia klabu hiyo ambayo inalenga kuwanyanyua na kuwafikisha mbali.

Aidha, George aliwataka wadau na wazazi kutoa sapoti ya kutosha ili kufanikisha zoezi hilo la kusaka vipaji kwa kuwa ni sehemu ya ajira wanazozitengeneza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.