Juhudi, Kibanda ‘out’ Kombe la UFA

Bingwa - - HABARI - NA VALERY KIYUNGU

TIMU za soka za Juhudi na Kibanda, zimetolewa katika mashindano ya Kombe la UFA yanayoendelea kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam.

Kikosi cha Juhudi kiliyaaga mashindano hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Soka Wilaya ya Ubungo (UFA), baada ya kufungwa bao 1-0 na Mbezi Kombaini.

Bao pekee la Mbezi Kombaini lilifungwa na Moshi Mrisho katika dakika ya 62 kwa shuti kali lililopigwa kutokea pembeni.

Kibanda FC ilifungwa mabao 2-1 dhidi ya Sinza Boys, ambapo bao la kwanza la washindi lilifungwa na Kabunda Kabunda katika dakika ya 27, baada ya kuwatoka mabeki na kuachia shuti kali.

Hata hivyo, bao hilo halikudumu kwani dakika mbili baadaye, Sinza Boys waliongeza bao la pili kabla ya Joshua Joel kuifungia timu yake ya Kibanda bao la kufutia machozi.

Mashindano hayo yanayolenga kuibua na kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi, yanashirikisha timu 32.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.