Ringo ataka wazee wajifunze karate

Bingwa - - HABARI - NA GLORY MLAY

RAIS wa Shirikisho la Karate Tanzania (TSKF), Sensei Willy Ringo, amewataka wazee kujifunza mchezo huo ili wapate ukakamavu na kuepuka uwezekano wa kuugua mara kwa mara uzeeni.

Akizungumza na BINGWA jana, Ringo alisema mchezo huo una faida kwa wazee kwani utasaidia kuimarisha afya zao na kuwafanya wenye nguvu licha ya umri wao kuwa mkubwa.

“Mimi ni mtu mzima, lakini kutokana na mchezo huu naonekana bado kijana, mazoezi yananipa furaha muda wote na yananiepusha na mawazo, nawashauri wazee wajifunze mazoezi haya yatawasaidia hata kuondokana na magonjwa ya uzeeni,” alisema Ringo.

Aidha, Ringo aliongeza kuwa mchezo huo unasaidia kujenga afya na kupunguza uzito na unene, hivyo ni mzuri zaidi kwa wazee kujifunza.

Alisema malengo yake ni kuhakikisha kila rika linashiriki katika mchezo wa karate kwani husaidia kutengeneza faida nyingi mwilini.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.