Garcia ajitetea kumchezesha kimeo Payet

Bingwa - - WEEKEND SPORT -

KOCHA wa timu ya Marseille, Rudi Garcia, amesema uamuzi wake wa kumwanzisha Dimitri Payet kwenye fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Atletico Madrid ulikuwa sahihi na ni kwa sababu ya uwezo wake wa hali ya juu.

Hata hivyo, Payet hakudumu kwa muda mrefu katika mtanange huo. Maumivu ya nyama za paja lake la kulia yalimlazimu atoke nje ya uwanja dakika ya 32 tu, huku akibubujikwa na machozi.

Iliripotiwa kuwa, Payet alianzishwa kwenye mchezo huo baada ya kuonekana yuko fiti kucheza fainali hiyo, lakini baada ya Marseille kutandikwa, Garcia alikiri staa wake huyo hakuwa vizuri, lakini aliamini kipaji chake ni silaha tosha.

“Nilimchagua Payet, mmoja wa wachezaji wetu bora. Nadhani mlikuwa mashahidi namna alivyofanya kazi kubwa kabla ya kutoka. Asubuhi ya leo (juzi), Payet hakutaka kufikiria kama aliumia sana na alihitaji kucheza,” alisema Garcia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.