Mmiliki kuiuza Newcastle kwa pauni mil. 400

MIKE Ashley, ambaye ni mmiliki wa klabu ya Newcastle United, ameripotiwa kuiweka timu hiyo sokoni na itapatikana kwa dau la pauni milioni 400, bei ambayo huenda ikakosa mteja.

Bingwa - - WEEKEND SPORT -

Mwaka jana alijitokeza mwanamama, Amanda Staveley, aliyetaka kuinunua klabu hiyo, lakini kutokana na bei hiyo, huenda mfanyabiashara huyo akajiondoa kwenye mpango huo.

Staveley na kampuni yake ya PCP Capital Partners waliripotiwa kukaribia kuinunua Newcastle kwa zaidi ya pauni milioni 300 kabla ya mazungumzo na Ashley kuvunjika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.