HIYO MADRID YA POCHETTINO ACHA KABISA

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

KIBARUA cha Zinedine Zidane §hakionekani kuwa salama kiasi hicho licha ya kuipa timu hiyo mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wakati huo huo, tayari Mauricio Pochettino, ameanza kutajwa kuwa ndiye atakayekalia kiti cha Mfaransa huyo.

Pochettino amezikoleza tetesi hizo kwa kile alichokifanya hivi karibuni, ambapo aliwaambia mabosi wake wa Spurs kuwa wamwongezee mshahara.

Wachambuzi wameibuka na aina ya kikosi cha Madrid chini ya kocha huyo, ikizingatiwa kuwa lazima atasajili wachezaji wake na hata kuachana na baadhi ya atakaowakuta.

DAVID DE GEA Alikaribia kwenda Madrid mwaka 2015 lakini ikashindikana katika dakika za majeruhi kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Ni wazi Pochettino ataufufua mpango huo, ikizingatiwa kuwa mlinda mlango wa sasa, Keylor Navas, ana umri wa miaka 30.

Kama alivyo Pep Guardiola, Pochettino, naye anapenda kipa anayechezea mpira kama aliyenaye sasa katika kikosi cha Spurs, Hugo Lloris.

ALEX SANDRO Ndiye Pochettino atakayemtazama kama mrithi wa Marcelo mwenye umri wa miaka 30. Atagharimu kama euro milioni 65 hivi.

Pochettino anapenda beki anayeshambulia, ni kama alipokuwa Southampton alipokuwa akimtumia Luke Shaw au Danny Rose aliyenaye Spurs.

MARCO VERATTI Ni mrithi sahihi wa Luca Modric licha ya kwamba Madrid watalazimika kuipiga bao Barcelona inayomtaka.

Rais wa Madrid, Fiorentino Perez, amekuwa akivutiwa naye, hivyo haitakuwa ngumu kwa Pochettino kusema aletewe kikosini.

NEYMAR Hata bila Pochettino, Madrid wamepania kumsajili Neymar, wakitajwa kutenga euro milioni 300.

Perez ni shabiki mkubwa wa Neymar ambaye kuna tetesi kuwa yuko tayari kuachana na Cristiano Ronaldo.

Hivi karibuni, mkongwe wa Brazil, Ronaldo, alimtaka Neymar kwenda Madrid.

EDEN HAZARD Licha ya kusema kuwa anafurahia maisha Chelsea, ukweli ni kwamba winga huyo anavutiwa na tetesi za kutakiwa mara kadhaa na Madrid.

Suala la kwenda kuwa mrithi wa Ronaldo au Gareth Bale si jambo ambalo kila mchezaji anaweza kulikataa.

Faida kubwa atakayokuwa nayo Pochettino ni kwamba msimu ujao, Chelsea hawatakuwa Ligi ya Mabingwa, hivyo huenda akatumia nguvu ndoto tu kumwambia Hazard kuwa si mchezaji wa kiwango cha Ligi ya Europa.

HARRY KANE Madrid kumchukua Pochettino watakuwa wameua

ndege wawili kwa jiwe moja. Iko hivi, kwanza watakuwa wamepata kocha. Pia, itakuwa rahisi kwao kumvuta Harry Kane ambaye wamekuwa wakimtolea macho.

Mwingereza huyo, Kane, amekuwa moto wa kuotea mbali chini ya Pochettino na misimu miwili iliyopita alimaliza ligi akiwa na mabao yaliyovunja rekodi ya Lionel Messi.

Kiasi cha euro milioni 2 00 kinatosha kabisa kwa Madrid kuina hivyo kuziba pengo la Kasa saini yake, ambaye kiwango chake krim Benzema hakitabiriki.

oja. Iko hivi, pata kocha. kumvuta ekuwa

e, amekuwa ini ya wili iliyopita bao nel Messi. 00 kinatosha sa saini yake, rim Benzema imekuwa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.