CHUKUA DONDOO KALI ZA KUBASHIRI WIKIENDI HII

Bingwa - - IJUMAA SPESHO - USICHANE MKEKA 0712029274

NI mechi chache tu zilizosalia kabla ya kumalizika kwa msimu huu na kuukaribisha msimu wa Kombe la Dunia. Nini nimekuandalia leo? Tembea na mkeka huu…

CHELSEA VS MAN UNITED Timu hizo zitatunishiana misuli kwenye fainali ya Kombe la FA kesho katika Dimba la Wembley, ukiwa ni mchezo wa mwisho kwa kila kocha wa timu hizo kuhakikisha analinyakua taji hilo na kumaliza msimu kwa furaha.

Chelsea itabidi wawe makini na rekodi ya Man United ya kushinda mechi saba mfululizo za mashindano ya kuwania kombe walizocheza kwenye Dimba la Wembley, wakati wao wakiwa na takwimu mbovu katika siku za hivi karibuni ambayo ni kushindwa kufunga bao katika mechi zao tatu kati ya nne za hivi karibuni katika michuano yote. Utabiri: Chelsea 0-1 Man United

VILLARREAL VS REAL MADRID Mechi hiyo itakuwa ni ya mwisho kwa Real Madrid kabla ya kuchuana na Liverpool wikiendi hii kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kimsingi wanaweza wakacheza katika namna tofauti na waliyozoeleka dhidi ya Villarreal.

Ni wazi Madrid hawatahitaji wachezaji wao wengine waumie tena, hivyo mastaa watapumzishwa na hilo litaikaribisha Villarreal ikawashambulie kwa kasi.

Utabiri: Villarreal 2-2 Madrid

LEGANES VS REAL BETIS Leganes wana shughuli kubwa ya kufanya kwani wanaelekea kushuka daraja licha ya kwamba katika kipindi cha hivi karibuni, walicheza soka la kiwango cha hali ya juu.

Watakutana na Betis huku wakiwa hawajashinda mechi zao tano za mwisho kwenye LaLiga, wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara mbili kila mechi. Wapinzani wao wamepoteza mechi moja tu kati ya 10 za mwisho kwenye ligi.

Utabiri: Leganes 1-2 Betis

CAEN V PSG Kwa sasa vinara wa Ligue 1, PSG hawana cha kupoteza. Wameshalinyakua taji la ligi hiyo na watakabiliwa na jukumu la kuhimili presha ya Caen ambayo ni timu inayojiengua na janga la kushuka daraja.

Hata hivyo, PSG imefungwa mara moja tu katika mechi 14. Na huenda ikawa ni mechi yenye mabao mengi pande zote kwani PSG wamefunga katika mechi tisa kati ya 10 za mwisho, Caen wamefunga mara sita kati ya 10.

Utabiri: Caen 2-2 PSG LYON V NICE Klabu mwenyeji itaikaribisha Nice kwenye dimba ambalo ndugu yao Marseille, alitandikwa na Atletico kwenye fainali ya Ligi ya Europa, je, itakuwa ni nuksi au hakutakuwa na tofauti yoyote hivyo wataendeleza vichapo? Changamoto kwa Nice ni kuhakikisha wanaifunga Lyon ambayo ikiwa kwake ni timu imara na isiyofungika kirahisi.

Lyon wanasaka nafasi ya kucheza Ulaya, Nice wanataka kubaki Ligue 1. Mara ya mwisho Lyon wanakutana na Nice walipata ushindi, lakini katika miaka ya hivi karibuni hawakuonesha kiwango kikali. Baada ya kutandikwa mwishoni mwa mwaka 2017, Nice haikufungwa tena kwenye mechi tano dhidi ya Lyon, tatu kati ya hizo walishinda.

Utabiri: Lyon 2-0 Nice

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.