Mkongwe Ujerumani astaafu baada ya kutemwa

Bingwa - - MAKALA | HABARI -

STRAIKA wa Bayern Munich, Sandro Wagner, ameamua kustaafu kuitumikia timu ya Taifa ya Ujerumani, baada ya kutojumuishwa katika kikosi cha wachezaji 27 watakaoliwakilisha taifa hilo kwenye fainali za Kombe la Dunia mapema mwezi ujao.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, amefunga mabao matano katika mechi nane za kimataifa alizoitumikia Ujerumani mapema mwaka huu.

Akizungumza kupitia jarida la Bild nchini Ujerumani, Wagner alisema anafikiria kustaafu kuitumikia timu hiyo. "Nimesikia (kutoitwa timu ya taifa) na nitastaafu kuitumikia Ujerumani, nadhani sina sifa za kucheza chini ya kocha Joachim Low. Siku zote mimi nipo wazi, kwa hili limeniuma,” alisema Wagner.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.