Neymar: Nalitaka Kombe la Dunia

Bingwa - - MAKALA | HABARI -

NYOTA wa timu ya Taifa ya Brazil, Neymar Jr, ameonyesha tamaa yake ya kuchukua ubingwa wa Kombe la Dunia Urusi, kwa mara ya kwanza ndani ya jezi ya timu yake hiyo tangu walipolitwaa mwaka 2002.

Ukiwa umebaki mwezi mmoja fainali hizo kuanza kutimua vumbi, staa huyo wa PSG ambaye anapambana kuwa fiti kurudi katika ubora wake, alisema ni jambo zuri kunyakua taji la michuano hiyo mikubwa duniani.

“Mashindano ya Kombe la Dunia ni makubwa, nataka kucheza na kuchukua ubingwa,” alisema.

“Hili kombe (kama) ni langu! Ninachopenda zaidi ni kucheza soka, nikiwa uwanjani nakuwa mtu mwenye furaha zaidi,” aliongeza.

Kitendo cha Neymar kurejea mazoezini wiki iliyopita kilileta faraja kwa nyota huyo kuwa huenda akaitumikia Brazil kwenye fainali hizo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.