Chelsea walipishwa mil 61/-

Bingwa - - HABARI -

CHAMA cha Soka cha England (FA), kimeitoza faini ya pauni 20,000 (zaidi ya Sh milioni 61 za Tanzania) klabu ya Chelsea, sababu ikiwa ni mchezo wao wa sare ya bao 1-1 dhidi ya Huddersfield.

FA imejiridhisha kuwa wachezaji wa Chelsea, akiwamo Antonio Rudiger, walishinda kujizuia na hatimaye kumfanyia fujo mwamuzi Lee Mason na wasaidizi wake.

"Tukio hilo lilitokea kipindi cha kwanza wakati wa mchezo wa Huddersfield Town uliochezwa Jumatano ya Mei 9," ilisema taarifa ya FA.

Chelsea wameumaliza msimu huu wa Ligi Kuu England wakiwa nafasi ya tano, nyuma ya Liverpool baada ya kutandikwa mabao 3-0 na Newcastle United katika mchezo wa mwisho.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.