Akanusha kucheza akiwa majeruhi

Bingwa - - HABARI -

STEPHEN Curry wa Golden State Warriors ya Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA), amesema si kweli kwamba alicheza akiwa majeruhi dhidi ya Houston Rockets.

Mchezo huo wa juzi uliwashuhudia Warriors wakiangukia pua kwa kichapo cha pointi 127-105.

Curry hakuwa katika ubora wake siku hiyo, kwani alimaliza mtanange huo akiwa ametupia pointi 16 pekee.

Mshindi huyo mara mbili wa tuzo ya Mchezaji Bora (MVP), amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti msimu huu lakini anaamini alikuwa fiti dhidi ya Rockets.

Kwa upande wake, Kocha wa Warriors, Steve Kerr, alisema kikosi chake hakikupambana vya kutosha kama walivyofanya wenzao hao. Uwanja wa NRG Stadium upo katika mji wa Houston, nchini Marekani na uwezo wake unachukua watazamaji, 71,054. Uwanja huu ambao huwa unatumiwa na timu ya taifa ya nchi hiyo na pia huwa unatumiwa na klabu ya Houston Dynamo kwa ajili ya mechi zake za ndani na za kimataifa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.