Rooney kununua nyumba jirani na Obama

Bingwa - - HABARI -

HUKU kukiwa na tetesi za kwenda kukipiga Marekani, Wayne Rooney ameziongezea nguvu kwa kutaka mjengo nchini humo.

Imeelezwa kuwa nyumba anayoitaka mwanasoka huyo iko Washington na ni katika mtaa anaoishi Rais wa zamani wa Marekani, Barrack Obama.

Ili kuipata, Rooney atalazimika kutoa pauni milioni 4.2 na ni mjengo wenye vyumba vingi vikiwamo saba vya kulala tu.

Mbali na Obama, Rooney mwenye umri wa miaka 32, atakuwa karibu na Ivanka Trump ambaye ni binti wa Rais wa Marekani, Donald Trump.

Baba huyo wa watoto watatu, anatarajiwa kuikimbia Everton ikiwa ni miezi 12 pekee imepita tangu alipojiunga nayo akitokea Manchester United.

Tofauti na akina David Beckham na Steven Gerrard ambao walipokwenda Marekani waliamua kuishi Los Angeles, Rooney ameamua kwenda kuweka makazi yake Washington.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.