Kaizer Chiefs wazima sherehe kisa kuukosa ubingwa

Bingwa - - HABARI -

HAKUNA sherehe za utoaji tuzo kwa wachezaji waliofanya vizuri klabuni hapo msimu huu kwa kuwa Kaizer Chiefs imeshindwa kuchukua ubingwa.

Timu hiyo ya mjini Johannesburg, ilimaliza mbio za ubingwa ikiwa nafasi ya tatu, ukiwa ni msimu wake wa tatu mfululizo kuambulia patupu.

Badala ya utamaduni wao wa kupongezana kwa tuzo ikiwamo ile ya mchezaji bora katika kikosi chao, watautumia muda huo kuangalia makosa yao na kujipanga kwa msimu ujao, ikiwamo kusaka kocha mpya.

"Uamuzi wetu umetokana na kukerwa na kiwango cha timu," alisema mwenyekiti wa timu hiyo, Kaizer Motaung.

Chiefs hawajalitia mkononi taji la Ligi Kuu tangu walipofanya hivyo mwaka 2015.

Tayari wana kibarua cha kusaka kocha mpya baada ya Steve Komphela kubwaga manyanga baada ya kikosi chake kutandikwa mabao 2-0 na Free State Stars, katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Nedbank.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.