Marseille waendeleza nuksi Europa...

AKIWA katika ardhi ya nyumbani, juzi Maresille walishindwa kulibeba taji la Ligi ya Europa baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0, katika mchezo wa fainali dhidi ya Atletico Madrid.

Bingwa - - SPORTS EXTRA -

WAlikuwa ni Antoine Griezmann aliyepachika mawili kabla ya nahodha wake, Gabi, kuweka jingine lililowamaliza kabisa Wafaransa hao.

"Nimefurahi sana. Nimekuwa nikilihangaikia hilo kwa miaka mingi,” alisema Griezmann. Kupoteza mchezo wa juzi uliochezwa mjini Lyon ni mwendelezo wa Marseille kuambulia patupu katika fainali zake zote tatu zilizopita za Ligi ya Europa.

Pia, kufungwa na Atletico kunamaanisha kuwa Marseille wameshindwa kumaliza uteja wa timu za Ufaransa katika michuanio hiyo kwani hakuna iliyowahi kutwaa ubingwa.

Ukiacha hilo, ilikuwa siku mbaya kwa mashabiki wa soka wa Ufaransa kwani kwa mara zote tano, sasa timu zao zimechakazwa na Wahispania.

Hali ilikuwa tofauti kwa wenzao wa Hispania ambao walishangilia taji lao la nane la michuano ya Ulaya (Ligi ya Mabingwa na Europa) tangu msimu wa 2013-14.

Hata hivyo, huku Griezmann akiibuka nyota wa mchezo, wachambuzi wa soka barani Ulaya wanaamini huenda mambo yangekuwa tofauti endapo Dimitri Payet angeendelea kuwa uwanjani.

Staa huyo amekuwa mwiba mkali kwa timu pinzani msimu huu, lakini juzi alicheza kwa dakika 30 pekee kabla ya kushindwa kuendelea na mchezo kutokana na maumivu ya nyama za paja.

Licha ya kazi nzuri katika eneo la kiungo, Payet ameifungia Maresille mabao sita ya Ligi Kuu (Ligue 1), huku akiwa na ‘asisti’ zake 22 katika mechi za michuano mbalimbali.

Griezmann naye amehusika katika mabao 12 ya Atletico msimu huu wa Ligi ya Europa, akifunga nane na kutoa asisti nne.

Kwa upande mwingine, amechangia asilimia 45 ya mabao yote ya timu hiyo (94), akiwa amefunga 29 na asisti 13.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.