WENGER AJUTA KUTOMSAJILI RONALDO

OCHA Arsene Wenger anaamini angekumbukwa zaidi katika historia ya Arsenal endapo angemsajili Cristiano Ronaldo mwaka 2004.

Bingwa - - MBELE -

KKipindi hicho Gunners walipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Ronaldo, lakini walizubaa na nyota huyo akatimkia zake Manchester United kwa pauni milioni 12.

Ronaldo akaipa Man United mataji nane, yakiwamo matatu ya Ligi Kuu England na kisha Real Madrid kumchukua kwa ada iliyovunja rekodi ya usajili duniani (Pauni milioni 80).

"Mchezaji ambaye tulimkosa na huwa ananijia akilini ni (Cristiano) Ronaldo," alisema Wenger.

"Alikuwa hapa na mama yake tulikuwa karibu mno. Man United wakaja kipindi ambacho walikuwa na kocha Carlos Queiroz.

“United walipocheza na Sporting Lisbon na Ronaldo akang’ara, ndipo walipomchukua,” aliongeza Wenger.

Wenger alisema Arsenal ingekuwa moto wa kuotea mbali endapo Ronaldo angetua na kucheza na Thierry Henry ambaye alikuwa mtambo wa mabao klabuni hapo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.