Klopp ateta na wakala wa Pogba

KOCHA Jurgen Klopp amezungumza na wakala anayetesa barani Ulaya ambaye mbali na mastaa wengine, pia anamsimamia Paul Pogba.

Bingwa - - SPORTS EXTRA -

Huyo ni Mino Raiola na imeelezwa kuwa kilichowakutanisha ni Klopp kutaka wachezaji wawili kwa ajili ya kikosi chake msimu ujao.

Raiola anamsimamia kipa wa AC Milan, Gianluigi Donnarumma, kinda wa Ajax, Justin Kluivert ambao Klopp amepanga kuwasajili katika dirisha la usajili la kiangazi litakalofunguliwa mwezi ujao.

Klopp hajakunwa na kikosi chake licha ya kwamba kimejihakikishia ‘top four’ msimu huu, huku kikiwa na mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Huku Naby Keita akiwa njiani kuelekea Anfield, imeripotiwa kuwa kocha huyo anataka kuiona Liver ikichukua taji la Ligi Kuu England msimu ujao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.