GWIJI LIVERPOOL AWACHANA MANE, SALAH, FIRMINO

Bingwa - - MBELE - MERSEYSIDE, England

MMartial amuweka

CHEZAJI wa zamani wa timu ya Liverpool, John Aldridge, njiapanda ameonesha Mourinho kutoridhishwa na kiwango cha nyota watatu wa Anfield, Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane na kudai ni kama vile si mafowadi waliotisha msimu uliopita.

Ushirikiano wa nyota hao ulikuwa ni silaha hatari ya Liverpool msimu uliopita, ambapo kwa pamoja waliweza kufunga jumla ya mabao 91 katika michuano yote, huku Salah akifunga mabao 44 peke yake.

Hata hivyo, msimu huu hawaonekani kama wataendeleza makali yao hayo, ambapo hadi sasa wameweza kutikisa nyavu mara 10 tu na Aldridge aliyeifungia Liverpool mabao 63 enzi zake za kusakata soka, alikiri kuwa msimu huu watatu hao wamepungua kasi.

“Kwa kiasi fulani safu ya ushambuliaji ya Liverpool imepungua kasi, Salah, Firmino na Mane hawaoneshi kile kiwango cha msimu uliopita,” alisema Aldridge.

“Sijui ni kitu gani kimewakumba watatu hao, natamani nikijue. Wamebadilika kwa kiasi kikubwa sana, kutoka msimu uliopita hadi huu, si washambuliaji tuliowazoea. Kwa wanaofahamu uwezo mkubwa walionao, ni wazi watakuwa wanaombea wasiendelee kuwa butu namna hii. “Kwa mfano Salah, kama unakumbuka msimu uliopita alikuwa si mtu wa kukosa nafasi moja kati ya mbili za wazi,” aliongeza.

“Nafahamu kuwa kocha wao, Jurgen Klopp, anajaribu kuwatafutia njia za kurudisha viwango vyao, lakini najua ni kitu kigumu sana, huenda kikawa kinamvuruga akili. Pengine msimu huu umekuwa ni mgumu sana kwao.

“Ukitazama namna Salah anavyokabwa na watu hadi wanne, unatarajia kumwona akitafuta njia nyingine ya kurahisisha mambo. Ukiwa straika unatakiwa kuanza kutafakari kwa kina kwanini haufungi tena, je, magoli yamekuwa madogo au makipa wana miili mikubwa siku hizi?” alihoji Aldridge.

“Kwa kiasi fulani safu ya ushambuliaji ya Liverpool imepungua kasi, Salah, Firmino na Mane hawaoneshi...

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.