Mkazi wa Mbezi Louis abeba bajaj ya SportPesa

Bingwa - - HABARI / TANGAZO - NA MWANDISHI WETU

MKAZI wa Mbezi Louis, Dar es Salaam, Alphonce Boniphace, amekabidhiwa zawadi yake ya bajaj aliyoshinda baada ya kufanikiwa kubashiri michezo kadhaa ya soka kwa kupitia kampuni ya SportPesa.

Baada ya kukabidhiwa zawadi yake hiyo, Boniphace alijawa na furaha isiyo kifani, akiamini bajaj hiyo itamwezesha kuboresha maisha yake kwa kiasi kikubwa baada ya kuhaha kwa muda mrefu akifanya kazi katika duka la vifaa vya ujenzi kama mwajiriwa.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa bajaj yake mpya, Boniphace alisema hii kwake ilikuwa ndoto ambayo mara kadhaa kwa kipato alichokuwa anapata kila siku kisingemwezesha yeye kununua bajaji, ila amepagawa baada ya kuona ndoto hii imekuwa kweli na kukamilishwa na SportPesa.

Mshindi huyo anaelezea kuwa, ni Sh 3,000 ndiyo imempa ushindi, ikiwa ni mara baada ya kutupia ubashiri wake kwa kutumia njia ya ussd, yani alibofya *150*87# akaweka ubashiri na kupokea ujumbe kupitia simu yake ndogo ya mkononi ukimtaarifu kuwa ameingia kwenye droo ya kushinda bajaj.

“Kuna wakati nilishawishika baada ya kumuona rafiki angu Pascal ambaye ndiye alikuwa mwalimu wangu na kunifanya niijue SportPesa akicheza na kushinda pesa, ndipo na mimi nikajisajili na kuanza kucheza, kikubwa nilikuwa nataka bajaj maana niliona kwenye mtandao wenu vile watu wanashinda nikajua na mimi ipo siku yangu, nimefurahi sana jamani, yani hata nashindwa kuongea,” alisema Boniphace.

Kwa kutumia simu yoyote ya mkononi unapiga *150*87# au unacheza kupitia tovuti www. sportpesa.co.tz., kumbuka ili ucheze ni lazima uweke pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa, namba ya kampuni ni 150888 na kumbukumbu namba ni 888, unapocheza mara nyingi zaidi ndio unaongeza nafasi ya kushinda.

Mshindi wa promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa, Alphonce Boniphace, mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, akikabidhiwa funguo ya bajaji na mwakilishi kutoka SportPesa, Frank Charles Gibebe. Na Mpigapicha Wetu

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.