BEKI YANGA AIPA UBINGWA TPL

Bingwa - - HABARI -

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

BEKI wa zamani wa Yanga, Jumanne Shengo, amesema timu hiyo ina nafasi ya kuchukua ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), msimu huu.

Akizungumza na BINGWA jijini juzi, Shengo alisema Yanga wana kila sababu ya kutwaa ubingwa huo kutokana na kiwango bora kinachoonyeshwa na wachezaji wa timu hiyo.

Shengo ambaye aliwahi kuzichezea Coastal Union, Pan African, Tukuyu Stars na Al-Masri ya Oman, alisema sababu nyingine inatokana na matokeo ya timu hiyo ambayo hadi sasa imecheza michezo sita bila kufungwa.

Alisema kwa sasa wachezaji wanacheza wakiwa hawana wasiwasi wa aina yoyote tofauti na timu nyingine ambazo zimekuwa zikicheza kwa presha ya mashabiki na viongozi.

“Yanga ni bingwa, sababu kubwa imekuwa ni timu yenye bahati lakini pia inacheza kwa malengo, nyie chezeni wao wanaangalia matokeo mwisho wa mchezo yanakuwaje.”

Alisema pamoja na Yanga haikufanya usajili wa kutisha, lakini jambo la kufurahisha imekuwa ikipata matokeo mazuri.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.