Waamuzi 40 kufanya ‘cooper test’ Zenji

Bingwa - - HABARI - NA IBRAHIM MAKAME, ZANZIBAR

WAAMUZI 40 wanatarajiwa kufanya mtihani wa utimamu wa mwili ‘Cooper test’ utakaofanyika kesho kwenye Uwanja wa Amaan, kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu visiwani hapa.

Akizugumza na BINGWA juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Visiwani hapa, Muhsin Ali Kamara, alisema mtihani huo umeandaliwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA).

Kamara alisema katika zoezi hilo, waamuzi wataanza kupimwa afya leo kabla ya kesho kuanza kufanya mtihani wa utimamu wa mwili.

Kamara alisema kamati ya waamuzi imejipanga kuhakikisha wanakuwa na waamuzi wengi vijana wa soka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.