KMKM, Jamhuri kucheza fainali FA

Bingwa - - HABARI - NA IBRAHIM MAKAME, ZANZIBAR

TIMU za KMKM na Jamhuri zinatarajia kucheza fainali ya Kombe la FA, itakayochezwa Oktoba 13, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.

KMKM ilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga bao 1-0 Polisi Zanzibar katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa Uwanja wa Amaan.

Bao pekee la washindi hao lilifungwa na beki wa Polisi Zanzibar, Mwalim Ali, dakika ya 30 akiwa katika harakati za kuokoa hatari iliyoelekezwa langoni mwao.

Kwa upande wa timu ya Jamhuri, ilifanikiwa kutinga fainali baada ya kuifunga mabao 2-0 Wawi Star.

Bingwa wa Kombe la FA atacheza na JKU katika mchezo wa Ngao ya Hisani utakaochezwa Oktoba 18, mwaka huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.