Wushu wapanga kujitanua mikoani

Bingwa - - HABARI - NA GLORY MLAY

UONGOZI wa Chama cha Kung Fu za Kichina (WUSHU), umesema utahakikisha kila mkoa unakuwa na chama cha mchezo huo.

Akizungumza na BINGWA jana, rais wa chama hicho, Mwarami Mwitete, alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na baadhi ya mikoa haina vyama vya mchezo huo.

Mwitete alisema malengo yao ni kutaka vyama vya mikoa visimamie mchezo huo na kupata mafanikio.

“Tunakibarua kizito kuhakikisha kila mkoa tunakuwa na chama na timu, tupo katika mipango hiyo kuona ni jinsi gani mchezo huu utakuwa kwa kasi hapa nchini,” alisema Mwitete.

Alisema hadi sasa Dar es Salaam na Morogoro ni mikoa ambayo ina vyama vya mchezo huo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.