Simba Queens waanza kujifua

Bingwa - - HABARI - NA GLORY MLAY

WAKATI Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake Tanzania Bara ikitarajia kuanza mwezi ujao, timu ya Simba Queens imeanza mazoezi kujiandaa na msimu mpya.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Mkuu wa Simba Queens, Antony Makunja, alisema wameanza mazoezi mapema ili aweze kujenga kikosi bora.

Makunja alisema mazoezi hayo yanaendelea katika Uwanja wa Shule ya Msingi Buruguni, jijini Dar es Salaam.

Alisema katika programu yake amepanga kucheza michezo mingi ya kirafiki kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, ili kubaini ubora na mapungufu ya kikosi chake na baadaye kuyafanyia kazi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.