Jeshi Stars zachezea vipigo Nyerere Cup

Bingwa - - HABARI -

TIMU ya mpira wa wavu ya GSU ya nchini Kenya, jana iliichapa Jeshi Stars ya Tanzania kwa seti 3-0 katika michuano ya Nyerere Cup inayoendelea kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ulioanza kwa ushindani, GSU ilishinda seti ya kwanza kwa ponti 25-19, seti ya pili pointi 25-10 na seti ya tatu pointi 25-17.

Katika mchezo mwingine, timu ya wanawake ya Jeshi Stars ilichapwa seti 3-0 dhidi ya DIC kutoka Kenya, ambayo ilishinda pointi 25-21 katika seti ya kwanza, 26-24 seti ya pili na kumaliza seti ya tatu kwa pointi 25-19.

Timu ya Pentagon ya jijini Arusha nayo ilishindwa kutamba baada ya kufungwa seti 3-0 dhidi ya Mombasa Prisons ya Kenya, ambako katika seti ya kwanza walifungwa pointi 25-20, 25-22 na 25-12.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Mkuu wa timu za Jeshi Stars, Yusuph Mkarambati, alisema kufungwa michezo yao ya kwanza si kwamba wameshindwa, bali ni mwanzo wa kufanya vyema katika michezo ijayo.

“Huwezi kuihukumu timu kwa mchezo mmoja, mashindano yanaendelea na tunaamini tutachukua ubingwa msimu huu, japo ushindani umeanza kwa kishindo,” alisema Mkarambati.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.