NJE YA UWANJA Mayweather aponda kitendo cha Khabib

Bingwa - - MAKALA/HABARI -

BONDIA Floyd Mayweather, ameshangazwa na tukio alilofanya nyota wa UFC, Khabib Nurmagomedov, baada ya kumshinda Conor McGregor na kisha kuanzisha fujo kwa wapambe wa mpinzani wake huyo, akikiita kitendo hicho kisicho cha kiuanamichezo.

Khabib alimshinda McGregor katika pambano hilo la uzito mwepesi lililochezwa wikiendi iliyopita, lakini baada ya kutangazwa mshindi, alitoka nje ya ulingo na kutembeza makonde hadi kwa kocha wa McGregor, Danis, ambaye aliumizwa maeneo ya kichwani.

Tukio hilo huenda likamgharimu Mrusi huyo na adhabu ya kulipa faini, kupokonywa ubingwa wake huo na kupigwa marufuku ya kujihusisha na mchezo huo.

“Ujue huyo jamaa aliyepigana na McGregor simfahamu vyema, lakini kwa alichokifanya kwa kweli hakiendani na asili ya michezo. Kwa ninavyofahamu atapigwa faini kubwa sana. Nakumbuka nilivyozichapa na Zab Judah, kulikuwa na fujo kubwa ndani ya ulingo na ilibidi ilipwe faini. Mamilioni ya fedha,” alisema Mayweather.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.