Marcelo yupo tayari kwa kazi

Bingwa - - MAKALA/HABARI -

MADRID, Hispania

LICHA ya timu ya Real Madrid kumaliza ‘programu’ yao ya tatu ya mazoezi wiki hii bila wachezaji wao wa kimataifa, lakini taarifa ya beki wao wa kushoto, Marcelo kumaliza mazoezi yote ni nzuri kwa miamba hao wa

Hispania.

Mbrazil huyo alipona jeraha alilopata katika mechi yao dhidi ya Sevilla siku kadhaa zilizopita na alishiriki katika mazoezi yote na wenzake hivyo

anatarajiwa kurudi dimbani wikiendi ijayo wakati Madrid itakapochuana na Levante kwenye mchezo wa La Liga.

Tangu beki huyo aumie, Real Madrid haijaweza kupata ushindi katika mchezo wowote.

Nao wachezaji Dani Carvajal na Karim Benzema, hawakufanya mazoezi na wenzao juzi Jumatano kwani bado wanaendelea kuuguza majeraha huku Isco naye akiisubiri El Clasico, Oktoba 28.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.