Phil Foden apania ubingwa Euro 2020

Bingwa - - MAKALA/HABARI -

LONDON, England

KIUNGO wa timu ya taifa ya England, Phil Foden, amesema kuwa lengo lake ni kulisaidia taifa lake kunyakua ubingwa wa Euro mwaka 2020. Kinda huyo machachari wa klabu ya Manchester City, alitarajiwa kuanza kuitumikia timu ya vijana chini ya miaka 21 kwa mara ya kwanza katika mchezo w a kufuzu Euro 2019 dhidi ya Andorra usiku wa kuamkia leo.

Foden anakumbukwa kwa msaada wake mkubwa katika timu ya vijana England chini ya miaka 17 iliyotwaa Kombe la Dunia mwaka jana na sasa amepania kufanya kweli kwenye timu ya wakubwa.

“Tuliposhinda Kombe la Dunia la vijana nilifurahi sana, sitasahau. Kombe la Dunia ni kitu kikubwa sana, ila nataka nifanye hivyo na katika timu ya wakubwa,” alisema Foden.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.