HARMONIZE AIOKOA NDANDA FC SINGIDA

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

KLABU ya Ndanda FC, imemshukuru staa wa Bongo Fleva, Rajab Kahali ‘Harmonize’, kwa kulipia deni la malazi kiasi cha shilingi 3,000,000, walilokuwa wanadaiwa na Hoteli ya City Garden iliyopo Singida.

Klabu hiyo ambayo mwishoni mwa wiki iliyopita ilikuwa mkoani humo kushiriki mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya klabu ya Singida United, ilikumbwa na kadhia ya kuzuiwa kuondoka hotelini baada ya kushindwa kulipa deni hilo.

Kupitia ukurasa wao wa picha jana, Ndanda FC walimshukuru Harmonize na uongozi wake kwa kuwapa kiasi cha shilingi 3,500,000 ambazo watazitumia kwa ajili ya kulipa deni pamoja na nauli za kurudi nyumbani kwao Mtwara.

“Kwa niaba ya Ndanda SC tunamshukuru sana Harmonize kwa msaada wake wa kutupatia shilingi milioni 3 na laki 5 (3,500,000), ambazo zitasaidia timu kulipa deni la malazi hapa Singida na kusafiri kesho kurudi Mtwara, Mwenyezi Mungu amjalie kwenye majukumu yake ya kila siku,” walimshukuru Harmonize ambaye yupo nchini Marekani akiendelea na ziara yake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.