Pancho Latino kuagwa leo Dar

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

MWILI wa mtayarishaji nyota wa muziki nchini, Joshua Magawa ‘Pancho Latino’, unatarajia kuagwa leo katika Hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Gairo mkoani Morogoro kwa mazishi kesho. Akizungumza na Papaso la Burudani, msemaji wa msiba huo msanii Fareed Kubanda ‘Fid Q’, alisema ibada ya kuaga mwili itaanza leo saa nne asubuhi ikifuatiwa na ndugu, jamaa na mashabiki kumuaga kisha safari ya kuelekea nyumbani kwao Gairo itaanza.

“Tunaaga kesho (leo saa nne asubuhi) na baada ya hapo tutaanza kwenda Lugalo, pia ratiba ya kesho huko Morogoro itaanza saa nne asubuhi, watu wataaga mwili na kufuatia na mazishi saa nane mchana,” alisema Fid Q.

Miongoni mwa nyimbo kubwa alizowahi kutengeneza Pancho Latino ni Baadaye Sana (Mabeste), Baby Candy (Dully Sykes), Bye Bye, Show za Joh (Joh Makini), Msiache Kuongea, Nangoja Ageuke, Bado Nipo Nipo, Msiache Kuongea (AY na FA), Dar es Salaam Stand Up (Chid Benz), Amore (Baby Madaha), Closer (Vee Money), He we Go (Jux, Wakacha), Nimechokwa, Mdananda (Shetta), Kariakoo (Mataluma) na nyingine nyingi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.