HAPA NDIPO MESSI ANAPOMTOAUK23 UK16 JASHO RONALDO

Bingwa - - MBELE -

MOSCOW, Urusi

WACHEZAJI wawili wa Urusi, Alexander Kokorin na Pavel Mamaev, wanashikiliwa na chombo cha dola nchini humo wakihusishwa na tukio la kuwashambulia maofisa wa Serikali katika mgahawa mmoja jijini Moscow.

Ripoti iliyotolewa na mtandao wa habari wa Tass, ilisema kwamba wanasoka hao walihusika katika tukio hilo lililotokea mapema wiki hii na tayari Wizara ya Mambo ya Ndani Urusi imeanza kufanya uchunguzi.

Kamera za ulinzi katika mgahawa huo wa Arbat, uliopo Kusini Magharibi mwa Moscow, zilimnasa Kokorin ambaye aliiwakilisha timu ya taifa ya Urusi katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Kokorin ambaye anakipiga Zenit St. Petersburg, alionekana kuvaa sweta jeusi lenye kofia ya kichwani na alimtandika konde mwanamume mmoja aliyekuwa akipata kifungua kinywa kwenye kona ndani ya mgahawa huo.

Ripoti nyingine pia ya mtandao wa Gazeta ilisema kwamba, maofisa hao wa ngazi ya juu serikalini waliumizwa vibaya huku mmoja wao akipoteza jino na kuhitaji huduma ya hospitali.

Kwa mujibu wa wafanyakazi wa mgahawa huo, wachezaji hao walikuwa wamelewa na walitumia dawa za kulevya. Mtandao wa Gazeta ulimnukuu mwanasheria wa Urusi ambaye alisema kwamba kosa kama lililotendwa na wanasoka hao ni la miaka mitano jela.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.