TOP 10

Bingwa - - MAKALA/HABARI -

1Eto’o ni mzaliwa wa jijini Douala, Cameroon, miaka 37 iliyopita, akiwa amezichezea timu kubwa duniani, zikiwamo Chelsea, Barcelona, Inter Milan na Real Madrid, na kupata mafanikio makubwa Ligi ya ndani na Kimataifa.

2Mwaka 2010, Eto’o alifanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza kubeba ubingwa wa Ulaya mara mbili mfululizo, kupitia timu mbili za Barcelona na Inter Milan, alipokuwa akifundishwa na Guardiola na Mourinho.

3Pia nguli huyo wa soka wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon aliwahi kuwa na pasipoti ya Hispania iliyomwezesha kufanya kazi kwenye Umoja wa Ulaya bila kutambulika kama mchezaji wa kigeni.

4Eto’o amefanikiwa kufunga mabao 100 katika misimu mitano aliyotumia kuichezea timu ya Barcelona na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee wa Afrika kucheza mechi nyingi La Liga.

5Mwanandinga huyo pia ni mchezaji wa kwanza kufunga mabao kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na wanne juu ya wanasoka Marcel Desailly, Paul Sousa na Gerard Pique na kubeba ubingwa wa michuano hiyo mfululizo akiwa na timu tofauti.

6Straika huyo matata aliwahi pia kuwa kwenye Timu ya Taifa ya Cameroon na kuwawezesha miamba hao wa Afrika kutwaa taji la michuano ya Olimpiki iliyofanyika nchini Australia mnamo mwaka 2000.

7Pia ni miongoni mwa wachezaji wa Afrika aliyekuwa na mafanikio makubwa baada ya kubeba tuzo za mchezaji bora wa Afrika zaidi ya mara nne kwenye miaka ya 2003, 2004, 2005 na 2010.

8Eto’o aliwahi kushiriki kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Cameroon mara tatu, ikiwa pamoja michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mara mbili tu (ambayo ana rekodi ya kipekee ya kufunga mabao 18).

9Eto’o amebakia kuwa mfungaji bora wa timu ya Taifa yake ya taifa ya Cameroon baada ya kulitumikia Taifa lake hilo jumla ya mechi 112 za ushindani na kuifungia mabao

150Mwaka 2005 Eto’o alinukuliwa akisema kwamba ni heri akauze karanga kijijini kwao kuliko aichezee Chelsea, lakini miaka nane baadaye alikubali kutua katika klabu hiyo, akitokea katika timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.