ATAPATA

Bingwa - - MAKALA/HABARI -

Bwazi?

ADO kuna ubishi juu ya nani mkali kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi? Nini kinachoufanya mjadala huo uendelee wakati takwimu ziko

Ni kweli wanasoka hao wamekuwa wakipambanishwa kwa miaka 10 sasa, lakini makala haya yanakuchambulia rekodi tano za Messi ambazo huenda ikachukua muda mrefu kwa Ronaldo kuweza kuzivunja.

Kwanza, Messi anashikilia rekodi ya kufikisha mabao 50 ndani ya msimu mmoja wa Ligi Kuu. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina, alifanya hivyo katika mechi 37 za msimu wa 2011-12.

Ronaldo alikaribia kuifikia rekodi hiyo katika msimu wa 2014-15, lakini aliumaliza akiwa amezitikisa nyavu mara 48 katika mechi 35.

Pili, Messi ndiye mwanasoka pekee kuibeba mara nne mfululizo tuzo ya Ballon d’Or, akifanya hivyo kuanzia mwaka 2009 hadi 2012.

Awali, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na mkongwe wa soka la Ufaransa, Michel Platini, ambaye akiwa kwenye ubora wake wa kuzifumania nyavu

aliinyakua mara tatu mfululizo, kuanzia mwaka 1983 hadi 1985. Alichoweza Ronaldo hadi sasa ni kuiweka mkononi mara mbili mfululizo na hiyo ni mwaka (20132014 na 20162017).

Tatu, Messi ana rekodi ya kufunga zaidi ya mabao 60 ya michuano mbalimbali kwa misimu miwili mfululizo. Ronaldo hajaweza kufanya hivyo katika ligi zote mbili alizocheza (England na La Liga), ukiacha Serie A aliyojiunga nayo hivi karibuni. Katika msimu wa 2011-12, mkali huyo wa Barcelona alifunga mabao 60 katika mechi zake 55 na msimu uliofuata yaani 2014-15, akaweka mengine 61 akiwa ameshuka dimbani mara 54. Nne, Messi anabaki kuwa mchezaji pekee kuwa na ‘asisti’ nyingi katika mechi zinazozikutanisha Real Madrid na Barcelona, mchezo ambao kwa mashabiki wa soka ulimwenguni kote wanaufahamu kwa jina la ‘El Clasico’. Hadi anaondoka zake Madrid na kwenda Italia kujiunga na Juventus, Ronaldo alikuwa na asisti moja tu katika mitanange ya El Clasico, wakati mwenzake, Messi, ana 14. Tano, kwa kwenda zake Juve, Ronaldo ameshindwa kuivunja rekodi ya Messi ya kuwa mwanasoka pekee aliyeziona nyavu mara nyingi katika historia ya mechi za El Clasico. 9

UK

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.