PAPASO LA BURUDANI

Washindi 15 wa BSS kutafutwa leo Dar

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

BAADA ya shindano la Bongo Star Search (BSS) kuwapata washindi 18 kutoka katika mikoa mitatu nchini, leo washindi 15 wataanza kutafutwa katika Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Next Door ulioko Oysterbay.

Taarifa hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Jaji Mkuu wa BSS, Ritha Paulsen, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Katika maelezo yake, Paulsen aliitaja mikoa walikopatikana washindi hao 18 kuwa ni Arusha, Mbeya na Mwanza.

“Kwa ujumla, mchakato wa kusaka vipaji mikoani ulikuwa ni wenye mafanikio kwa sababu vijana wengi walijitokeza na kushiriki kwa hamasa.

“Yaani vijana wamekuwa na hamasa zaidi ya kuimba na kuonyesha uwezo wao kwenye fani ya muziki na majaji wenzangu hawakuishia tu kuwapitisha walioimba vizuri bali pia wale waliochemka tuliwapa ushauri zaidi ili wasikate tamaa ya kushiriki kwa siku zijazo.

“Nasema hivyo kwa sababu BSS imekuwa mstari wa mbele kuwasaidia vijana ili waone mwanga kwenye fani ya muziki ndiyo maana tumejipanga kuhakikisha tunawainua na kuwafikisha mbali kwenye fani hii ya muziki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.