Kocha NBA afariki

Bingwa - - HABARI -

ALIYEWAHI kuwa kocha msaidizi wa Chicago Bulls ya Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA), Fred 'Tex' Winter, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 96.

Kwa mujibu wa mkongwe, Michael Jackson, Winter, aliyeipa Chicago mataji sita ya Ligi Kuu hiyo, ndiye aliyemvutia kupenda mpira wa kikapu.

Hata alipotua Los Angeles Lakers, aliiongoza timu hiyo kutwaa mara tatu mfululizo ubingwa huo, kuanzia mwaka 2000 hadi 2002.

Akimzungumzia Winter, Mtendaji Mkuu wa Bulls, John Paxson, alisema: "Tex Winter hakuwa lejendari wa kikapu tu, pia alikuwa mwalimu muhimu katika historia ya mchezo huu."

Jordan naye alisema: "Nilijifunza mengi kutoka kwa kocha Winter na kwangu ni bahati kucheza chini yake…”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.