Henry anukia

Kocha Monaco atimuliwa

Bingwa - - HADITHI -

KLABU ya Monaco imethibitisha kumtimua kocha wao, Leonardo Jardim, ambaye alidumu na kikosi hicho kwa miaka minne na kuwapitia ubingwa wa Ligi Kuu Ufaransa, Ligue 1, msimu wa 2016/17.

Jardim amefukuzwa kwa sababu kikosi hicho kimeshindwa kufanya vizuri tangu kuanza kwa msimu huu, wakifanikiwa kushinda mchezo mmoja kati ya tisa iliyochezwa mpaka sasa.

Lakini taarifa ambazo zipo zinadai kuwa, Monaco imeanza mazungumzo na kocha msaidizi wa Ubelgiji, Thierry Henry, ambaye hivi karibuni alihusishwa na kibarua cha kuinoa timu ya Aston Villa.

soka na

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.