FDL, SDL Unguja zasimamishwa

Bingwa - - HABARI - NA IBRAHIM MAKAME, ZANZIBAR

KAMATI ya Rufaa na Usuluhishi ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), imesimamisha kwa muda Ligi Daraja la Kwanza Kanda (FDL) na Ligi Daraja la Pili Taifa (SDL) kisiwani Unguja.

Uamuzi huo umetolewa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa timu ya Miembeni City yanayoitaka kamati hiyo kusimamisha ligi hizo.

Kaimu Katibu wa ZFA, Khamis Abdallah Said, alisema wamepokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Takky Abdulla Habib, inayoeleza kwamba ligo hizo zimesimamishwa kwa muda mpaka watakapotoa uamuzi.

Aidha, alisema ZFA kupitia kamati hiyo ya rufaa na usuluhishi, wamejiridhisha na malalamiko yaliyotolewa na klabu ya Miembeni City kutokana na kushushwa daraja la pili Taifa msimu uliopita.

“ZFA ndiyo imeunda kamati hii hivyo hatuna budi kuhakikisha tunaipa nafasi ya kufanya majukumu yake, maana haki za klabu na wachezaji zinafanyiwa kazi kupitia kamati hii.

“Tunaomba klabu zitusamehe kwa uamuzi huu maana zilikuwa zimeshajiandaa, pia wale waliokuwa wameshatumia gharama zao waiandikie ZFA zitalipwa, rufaa itapokaposikilizwa ligi zitaendelea,” alisema.

Timu ya Miembeni City iligomea michezo mitatu ya Ligi Kuu Zanzibar msimu uliopita baada ya kushindwa rufaa yao dhidi ya klabu ya Chuoni na ZFA kuishusha madaraja mawili.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.