Griezmann, Atletico ‘ndoa’ haivunjiki

Bingwa - - DONDOO -

KLABU zinazoiota saini ya straika Antoine Griezmann zitafute kazi nyingine ya kufanya, kwani Mfaransa huyo amesema habanduki ng’o.

Kauli ya Griezmann kwamba anafurahia maisha pale Atletico ilikuja baada ya kufunga katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund, mchezo wa marudiano baada ya ule waliotandikwa 4-0 kule Ujerumani.

Kwa upande wake, kocha Diego Simeone alisema amekoshwa na kiwango cha mchezaji huyo, ingawa alisisitiza kuwa ni matokeo ya ushirikiano mzuri wa timu nzima.

"Yuko kwenye kiwango kizuri. Alikuwa tishio msimu uliopita,” alisema Simeone, mchezaji wa zamani wa Atletico na timu ya taifa ya Argentina.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.