MWANZA YATEUA 31 KIKAPU TAIFA CUP

Bingwa - - HADITHI - NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA

WACHEZAJI 31 wamechaguliwa kuunda timu ya wanaume ya Mkoa wa Mwanza itakayoshiriki katika michuano ya mpira wa kikapu Taifa (Taifa Cup), itakayofanyika hivi karibuni mkoani Simiyu.

Uteuzi huo umesimamiwa na Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Mwanza (MRBA), ambapo wachezaji wengi wanatokana na michuano ya ligi ya kikapu mkoani hapa iliyomalizika Oktoba, mwaka huu na timu ya Profile kuibuka mabingwa kwa mwaka wa nne mfululizo.

Akizungumza na BINGWA juzi jijini hapa, Mwenyekiti wa Mashindano wa MRBA, Haidari Abdul, alisema timu ya Profile imetoa wachezaji nane, Planet saba, Eagles watano, Octopus wanne, Cuhas wawili na Warriors mmoja.

Alisema kikosi hicho kilianza mazoezi jana (Jumatatno) kwenye viwanja vya kisasa vya Mirongo chini ya makocha, Paschal Nkuba na Kizito Bahati.

Wachezaji walioitwa kuunda timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Taifa Cup Simiyu 2018, ni Bashir Ashiraf, Nelson Mlawa, Amon Senberya, Lugina Laban, Fred Charles, Shaban Ally, Bassa Mponjoli, Abdallah Hamza, Peter Jangu na Malili Lubasha wote kutoka Profile.

Wengine ni Fransic Shilinde, Chacha Tubet, Joram Karugila, Mohamed Ally, Ahmed Mbega, Shomar Almas na John Pastory wote kutoka Planet, Ladslaus Lusato, Laurent Masatu, Gud Wambura, Chris Mapunda na Makuru Francis (Eagles).

Pia wamo Sam Kurongwa, Daniel Malaki, Roma Kisia na Denis Bilame (Octopus), Lamek Sosoka, Andrew Konga na Joseph Carlos (Cuhas), Vincent Shinda kutoka Spider na Emma John wa Warriors.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.