Zahera ataka ‘kufia’ Jangwani

Bingwa - - HABARI - NA TIMA SIKILO

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amefunguka kuwa hana mpango wakuondoka katika timu hiyo kwa sasa hata kama kuna timu itamhitaji kwa dau lolote.

Zahera ambaye ametua kwenye timu hiyo msimu huu akichukua mikoba ya George Lwandamina wa Zambia, ameweka wazi kwamba anafukuziwa na timu nyingi ikiwamo Builcon.

Zahera ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu yake ya Taifa ya DR Congo, akizungumza na BINGWA jana, alisema ni kweli timu ya Builcon kutoka Zambia ilionyesha nia ya kumhitaji tena kwa dau kubwa lakini hayupo tayari kuiacha Yanga kwa sasa.

Zahera alisema hayupo tayari kuvunja mkataba wake na Yanga kwa kuwa ameamua kuifundisha timu hiyo hadi mwisho.

“Ni mapema mno kuondoka Yanga, siwezi kuiacha Yanga kwa sasa, huwa

nawafundisha wachezaji wangu kuvumilia na kupambana, sasa kwanini niwakimbie mapema,” alisema Zahera.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.