Ruvu Shooting yawataka Mayanja, Zahir

Bingwa - - HABARI /TANGAZO - NA TIMA SIKILO

TIMU ya Ruvu Shooting imeweka wazi kuwa katika kuboresha kikosi chao kuelekea katika dirisha dogo la usajili, wana mpango wa kuwasajili wachezaji, Vitalis Mayanja wa Ndanda na Rajab Zahir, anayecheza Singida United.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya timu hiyo kililiambia BINGWA jana kwamba, kutokana na mapungufu ambayo timu imeyaona wapo katika harakati za kutaka kuinasa saini ya wachezaji hao, kwani wana imani kwa uwezo ambao wameuonesha kwa kipindi hiki wanaweza kuisaidia timu hiyo kwa asilimia kubwa.

“Ruvu Shooting tunatarajia kufanya usajili wa wachezaji watatu ambao ni Vitalis, Zahir na mwingine kutoka Stand United.”

Chanzo hicho kilisema bado uongozi wa Ruvu haujazungumza na mchezaji hata mmoja wala viongozi wao, hivyo wanasubiria muda mwafaka ufike waweze kufanya majadiliano hayo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.