Mng’ao Band yawaanika mastaa

Bingwa - - HABARI - NA BRIGHER MASAKI

BENDI inayokuja kwa kasi kwenye muziki wa Bongo Fleva, Mng’ao Music Band’, imewaanika mastaa na tabia zao mbalimbali katika wimbo wa Siyo Kweli ikiwa ni njia ya kutaka wajirekebishe.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Meneja wa bendi hiyo, Sefu Shaban ‘Kigo Billionea’, alisema umefika muda wa wasanii kukosoana wao kwa wao ili jamii isiharibike na matendo yanayofanywa na mastaa.

“Kwa sasa mimi ndiyo nawadhamini vijana ili nikuze vipaji vyao, kwa kuanza tumeona tutoe wimbo huu Siyo Kweli ambao unaelezea tabia za mastaa wetu na tukitaka wabadilike ili jamii yetu ipone,” alisema Kigo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.