HATA AZAM WASIPONILIPA NITASEPA

Bingwa - - HABARI -

katika dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kuanza Novemba 15, huku akitamba bado ana uwezo mkubwa kuliko awali na ili kuthibitisha hilo atahakikisha anaifungia timu yake mabao mengi.

Azam inayoongoza ligi ikiwa na pointi 30, inafanya maboresho kuelekea dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, linalotarajia kuanza Novemba 15, mwaka huu.

Mchezaji huyo ni miongoni mwa washambuliaji waliokuwa wakitegemewa na Wanajangwani katika misimu miwili iliyopita, kabla ya kukimbia njaa na kutimkia nchini Misri.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Chirwa, alisema amefurahi kusajiliwa hapo na anawaomba mashabiki wamwamini na kumwombea, huku akiahidi kufunga mabao 10 hadi kufikia mwisho wa msimu huu kama hakutakuwa na tatizo la malipo.

“Mimi nina familia, si kwamba Azam wasiponipa haki zangu nitaendelea kubaki hapa, hapana nitatoka kwenda kutafuta maisha,” alisema Chirwa.

Alisema kuna timu nyingi ambazo amezikataa na kuamua kuja kuitumikia Azam, ikiwemo AFC Leopards ya Kenya na nyingine kutoka nchini Morocco.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van der Pluijm, alisema anamwamini mchezaji huyo, huku akiweka wazi kuwa yeye ndio chanzo cha kurudi Tanzania, uwepo wake ndani ya safu yake ya ushambuliaji utaleta mabadiliko makubwa.

“Chirwa ni mchezaji ambaye hakati tamaa anapokuwa uwanjani na ana juhudi kubwa katika kuhakikisha anapata mabao, tofauti na wachezaji wengi ni mchezaji mzuri na ninamwamini,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.