Reha yajipanga kuipa dozi Namungo FC

Bingwa - - MAONI MTAZAMO KATUNI - NA GLORY MLAY

KOCHA mkuu wa timu ya Reha FC, Salum Kumbalatula, amesema wanajipanga vyema ili waweze kugawa dozi kwa Namungo FC katika mchezo wao wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) utakaopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Reha walishindwa kuondoka na pointi tatu dhidi ya Mlale FC katika mchezo huo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Kumbalatula alisema licha ya kupoteza mchezo huo lakini wataendelea kujituma uwanjani ili waweze kufanya vizuri katika mechi zinazofuata.

Aidha, alisema atafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita ili waweze kutimiza malengo yao.

“Tutapambana ili tusirudie makosa, tumedhamiria kupata matokeo mazuri maana tunahitaji kupanda daraja msimu huu, pia tutahakikisha hatupotezi mechi hata moja,” alisema Kumbalatula.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.