NYOTA FIORENTINA ATEMWA BURKINA FASO

Bingwa - - MAKALA/HABARI - WAGADUGU, Burkina Faso

KOCHA wa timu ya taifa ya Burkina Faso, Paulo Duarte, amemwacha kikosini kiungo wake anayeichezea Fiorentina ya Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’, Bryan Dabo.

Hata hivyo, Duarte raia wa Ureno hajaweka wazi sababu ya uamuzi wake huo wa kumnyima Dabo nafasi ya kuwafuata Angola katika mchezo wa kuwania kwenda Afcon 2019 utakaochezwa Novemba 18, mwaka huu.

Dabo mwenye umri wa miaka 26, ambaye anacheza eneo la kiungo wa ulinzi, aliitwa katika mechi zote zilizopita dhidi ya Mauritania na Botswana waliocheza nao mara mbili.

Ukiacha mchezaji huyo mwenye mechi 10 za msimu huu wa Serie A, kikosi cha Burkina Faso kitazikosa huduma ya fowadi wake anayeishi Ubelgiji, Banou Diawara, kutokana na majeruhi.

Adama Guira anayecheza Denmark, ambaye kwa mara ya mwisho aliichezea Burkina Faso Februari, katika mchezo walioshinda mabao 2-0 dhidi ya Guinea Bissau, amerejeshwa kundini.

Mauritania wako kileleni mwa Kundi I wakiwa na pointi tisa, wakati Burkina Faso wanafuata (7), huku Angola (6) wakishika nafasi ya tatu na Botswana wakiburuza mkia (1).

Kikosi kamili ni kama ifuatavyo: Makipa- Sanou Germais (Beauvais, Ufaransa), Harve Kouakou Koffi (Lille, Ufaransa), Aboubacar Sawadogo (Al Najoom, Saudi Arabia).

Mabeki- Edmond Tapsoba (Guimaraes, Ureno), Issouf Dayo (Berkane, Morocco), Steeve Farid Yago (Toulouse, France), Bakary Kone (Ankaragucu, Uturuki), Patrick Malo (Asec, Ivory Coast), Yacouba Coulibaly (Le Harve, Ufaransa), Jean Noel Lingani (Horoya, Guinea)

Viungo- Blati Toure (Cordoba, Hispania), Charles Kabore (Krasnodar, Russia), Sanogo Zakaria (TSV Hartberg, Austria), Cyrille Bayala (Lens, Ufaransa), Razack Traore (Konyaspor, Turkey), Adama Guira (AGF, Denmark), Souleymane Sawadogo (Levadiakos, Greece), Djibril Cheick Ouattara (ASFB, Burkina Faso)

Washambuliaji- Alain Trore (Berkane, Morocco), Ahmed Toure (Asec, Ivory Coast), Bertrand Traore (Lyon, Ufaransa), Jonathan Pitroipa (Paris FC, Ufaransa), Abou Ouattara (Mechelen, Ubelgiji), Souleymane Kouanda (Asec, Ivory Coast)

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.