Bayern: AEK wangekufa nyingi tu

Bingwa - - SPORTS - MUNICH, Ujerumani

NIKO Kovac anayeinoa Bayern Munich, amedai walistahili ushindi mnono zaidi na si ule wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya AEK Athens juzi usiku.

Katika mchezo huo, Bavarians walipata mabao yote mawili kupitia kwa straika wao hatari raia wa Poland, Robert Lewandowski.

"Tungeweza kufunga mabao mengi zaidi na kuumaliza mchezo mapema tu, lakini mwisho wa siku tulistahili kuondoka na pointi zote tatu,” alisema Kovac.

Matokeo hayo sasa yanaifanya Bayern kuhitaji pointi moja pekee katika mchezo wao ujao dhidi ya Benfica ili kujihakikishia safari ya kwenda hatua inayofuata ya 16 bora.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.