HAPA BATA TU!

Bingwa - - IJUMAA SPESHO - VIWANJA VYA MWEMBE YANGA – TEMEKE, DAR ES SALAAM

Kesho ndio litakuwa onyesho la mwisho la Muziki Mnene baada ya kutimua vumbi kwenye mikoa kama Tanga na mengineyo. Wasanii watakaotoa burudani katika onyesho hilo ni Snura Mushi, Sholo Mwamba, Ney wa Mitego, Tunda Man, Izzo Bizness, Amber Lulu na wengine kibao.

TRAVENTINE HOTEL- MAGOMENI

Leo kutakuwa na uzinduzi wa albumu ya Mama wa Hiari kutoka kwa Abubakari Sudi ‘Prince Amigo’ na kundi lake la First Class Modern Taarab, wakitarajiwa kusindikizwa na wakongwe kibao kama Khadija Kopa, Mwanaha Ally, Sabaha Salum, Rukia Ramadhani, Mwanamtama Amir na wengine wengi waliobobea katika muziki huo wa pwani.

TWANGA PEPETA

Kama kawaida ya Twanga Pepeta (African Stars International’ kila Jumamosi kwenye Ukumbi wa The Jonz Pub uliopo Magomeni Mwebechai ambapo watatoa burudani kwa kukonga mioyo ya mashabiki wao na wale wa muziki wa dansi kwa nyimbo zao mbili mpya za Wivu na Rekebisha. Jumapili watakuwa Club Legend eneo la Namanga, Msasani.

FRIENDS CORNER –MANZESE

Wikiendi hii Yah TMK Modern Taarab watatatoa burudani kwenye ukumbi huo wakiimba vibao vyao vipya na vile vya zamani.

CLUB LEGEND- NAMANGA MSASANI

Kila Ijumaa Banana Zoro na bendi yake ya B Band watakamua pamoja na Dj Cobo na Dj JD kwenye ukumbi huo wa Club Legend.

BELLAZ BAR- MBEZI JOGOO

Jumamosi hii kuanzia saa sita mchana kutakuwa na uzinduzi rasmi wa ‘live band’ ya baa hiyo hivyo chakula na vinywaji ikiwamo nyama choma na vingine vitatolewa bure hadi saa 12:00 jioni, baada ya hapo utalipia.

Pia bendi hiyo itaanza rasmi kazi kwa kushusha burudani kwa wateja wa baa hiyo ambapo watapiga nyimbo zao na zile za ‘kukopy’.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.