Vita ya wenye kwa wenyewe

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

NA MWANDISHI WETU

KESHO kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha kutakuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kundi la Weusi na Dogo Janja.

Kundi la Weusi linaloundwa na wasanii; Joh Makini, Niki wa Pili, G Nako, watapanda kwenye jukwaa moja la Tamasha la Tigo Fiesta na mkali wa wimbo wa Banana, Dogo Janja, wote ni wenyeji wa ukanda huo wa Arusha. Katika onyesho hilo la kesho ambalo linatarajiwa kuwa bab kubwa kutokana na maandalizi yaliyofanywa kwa muda wa wiki nzima, litapambwa na wasanii wengi, lakkini Weusi na Dogo Janja ndio wanatarajiwa kuonyeshana umwamba kwa mashabiki wa nyumbani kwao. Wasanii wengine wanaotarajiwa kupam jukwaa hilo la Tigo Fiesta ambalo mwakaba huu limepewa jina Fiesta Vibe Kama Lote ni Aslay, Nandy, Barnaba Boy na Bill Nass. Rostam (Roma Mkatoliki na Stamina) nao pia wataungana na akina Fid Q, Rosaree, Ben Pol, Mr Blue, Maua Sama na Belle 9, kuwaburudisha wakazi hao wa Arusha. Huu ni mkoa wa 11 kufanyika tamasha hilo la Fiesta kwa mwaka huu, baada ya kutimua vumbi Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Mwanza, Musoma, Kahama na Muleba. Katika onyesho la Kahama msanii wa Weusi, Joh Makini alikamua pamoja na Dogo Janja ambaye alichana kwenye wimbo wa Don’t Bother ambapo alivamia jukwaani na ‘kurap’ kipande cha msanii wa Afrika Kusini, AKA aliyeshirikishwa kwenye wimbo huo na kuibua shangwe kubwa kwa

mashabiki.

Hivyo baada ya kuwapagawisha mashabiki kwa ‘show’ bab kubwa waliyopiga kwenye onyesho hilo la Kahama, kesho watarudi tena jukwaani kwa mashabiki wao wa nyumbani na kuonyeshana kazi.

Baada ya onyesho hilo la Arusha, tamasha la Tigo Fiesta litakwenda Singida na Dodoma kisha kumalizikia jijini Dar es Salaam Novemba 24, mwaka huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.