PAPASO LA BURUDANI

Ericzine awakumbusha wasanii kusoma sanaa

Bingwa - - IJUMAA SPESHO - NA BRIGHTER MASAKI

MSANII wa muziki na mwanafunzi aliyehitimu masomo katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Eric Renatus ‘Ericzine’, amewashauri wasanii kusomea sanaa ili waweze kutoa kazi zitakazokuwa na maadili kwa jamii.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Ericzine alisema elimu aliyopata katika Taasisi hiyo inamuwezesha kufanya sanaa akiwa na uelewa mkubwa kiasi cha kutambua kazi ipi nzuri na ipi haifai kwa mashabiki.

“Naitumia elimu yangu ya sanaa kuwarekebisha na kuwaelekeza wasanii wenzangu, hasa mastaa ambao wamenitangulia kuwa wanaweza kufanya muziki au filamu na wakafikisha sanaa kwa hadhira bila kukiuka maadili na katiba ya nchi yetu,” alisema Ericzine, anayefanya vizuri na wimbo Anadeka.

Ericsize

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.