Martin Kadinda awaangukia mashabiki

Bingwa - - IJUMAA SPESHO - NA JEREMIA ERNEST

MWANAMITINDO na mbunifu wa mavazi, Martin Kadinda, amewaomba Watanzania kumpigia kura katika tuzo za The Man za nchini Nigeria katika kipengele cha Mbunifu Bora wa Kiume wa mwaka.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Kadinda alisema amefurahi kupata nafasi hiyo ya kuwawakilisha Watanzania katika tasnia ya mitindo, hivyo ni jukumu la kila mmoja kumpigia kura ili ashinde.

"Ninafurahi kuona mafanikio yakinikaribia, naomba Watanzania wenzangu wanipigie kura ili niweze kushinda tuzo hii ambayo itatangaza nchi yetu katika tasnia ya mitindo," alisema Kadinda.

Aliongeza kuwa, tuzo hizo zitakazotolewa Novemba 16 mwaka huu katika Hoteli ya Oriental jijini Lagos, zimeanza kupokea kura kupitia tovuti yao ya www.manmagazineng. com/vote .

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.